Native Bible

Jeremiah 2:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu ili mpate kula matunda yake na utajiri wa mazao yake. Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu, na kuufanya urithi wangu chukizo.

Jeremiah 2:7 in English

Jeremiah 2:7 · Berean Standard Bible

I brought you into a fertile land to eat its fruit and bounty, but you came and defiled My land, and made My inheritance detestable.

Context

5Hivi ndivyo asemavyo Bwana: “Je, baba zenu waliona kosa gani kwangu, hata wakatangatanga mbali nami hivyo? Walifuata sanamu zisizofaa, nao wenyewe wakawa hawafai. 6Hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana, aliyetupandisha kutoka Misri na kutuongoza kupitia nyika kame, kupitia nchi ya majangwa na mabonde, nchi ya ukame na giza, nchi ambayo hakuna mtu asafiriye ndani yake wala hakuna mtu aishiye humo?’ 7Niliwaleta katika nchi yenye wingi wa vitu ili mpate kula matunda yake na utajiri wa mazao yake. Lakini mkaja na kuinajisi nchi yangu, na kuufanya urithi wangu chukizo. 8Makuhani hawakuuliza, ‘Yuko wapi Bwana?’ Wale wanaoshughulikia sheria hawakunijua mimi; viongozi waliasi dhidi yangu. Manabii walitabiri kwa jina la Baali, wakifuata sanamu zisizofaa. 9“Kwa hiyo naleta tena mashtaka dhidi yako,” asema Bwana. “Nami nitaleta mashtaka dhidi ya watoto wa watoto wako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.