Yeremia 12:8
Jeremiah 12:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba wa msituni. Huningurumia mimi, kwa hiyo ninamchukia.
Jeremiah 12:8 in English
Jeremiah 12:8 · Berean Standard Bible
My inheritance has become to Me like a lion in the forest. She has roared against Me; therefore I hate her.
Context
6Ndugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe:
hata wao wamekusaliti;
wameinua kilio kikubwa dhidi yako.
Usiwaamini, ingawa wanazungumza
mema juu yako. 7“Nitaiacha nyumba yangu,
nitupe urithi wangu;
nitamtia yeye nimpendaye
mikononi mwa adui zake. 8Urithi wangu umekuwa kwangu
kama simba wa msituni.
Huningurumia mimi,
kwa hiyo ninamchukia. 9Je, urithi wangu haukuwa
kama ndege wa mawindo wa madoadoa
ambaye ndege wengine wawindao
humzunguka na kumshambulia?
Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni;
walete ili wale. 10Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu
na kulikanyaga shamba langu;
watalifanya shamba langu zuri
kuwa jangwa la ukiwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.