Yeremia 12:6
Jeremiah 12:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe: hata wao wamekusaliti; wameinua kilio kikubwa dhidi yako. Usiwaamini, ingawa wanazungumza mema juu yako.
Jeremiah 12:6 in English
Jeremiah 12:6 · Berean Standard Bible
Even your brothers— your own father’s household— even they have betrayed you; even they have cried aloud against you. Do not trust them, though they speak well of you.
Context
4Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini,
na majani katika kila shamba kunyauka?
Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu,
wanyama na ndege wameangamia.
Zaidi ya hayo, watu wanasema,
“Bwana hataona yatakayotupata sisi.” 5“Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda,
unawezaje kushindana na farasi?
Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama,
utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani? 6Ndugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe:
hata wao wamekusaliti;
wameinua kilio kikubwa dhidi yako.
Usiwaamini, ingawa wanazungumza
mema juu yako. 7“Nitaiacha nyumba yangu,
nitupe urithi wangu;
nitamtia yeye nimpendaye
mikononi mwa adui zake. 8Urithi wangu umekuwa kwangu
kama simba wa msituni.
Huningurumia mimi,
kwa hiyo ninamchukia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.