Native Bible

Jeremiah 12:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini, na majani katika kila shamba kunyauka? Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu, wanyama na ndege wameangamia. Zaidi ya hayo, watu wanasema, “Bwana hataona yatakayotupata sisi.”

Jeremiah 12:4 in English

Jeremiah 12:4 · Berean Standard Bible

How long will the land mourn and the grass of every field be withered? Because of the evil of its residents, the animals and birds have been swept away, for the people have said, “He cannot see what our end will be.”

Context

2Umewapanda, nao wameota, wanakua na kuzaa matunda. Daima u midomoni mwao, lakini mbali na mioyo yao. 3Hata hivyo unanijua mimi, Ee Bwana; unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa! Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa! 4Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini, na majani katika kila shamba kunyauka? Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu, wanyama na ndege wameangamia. Zaidi ya hayo, watu wanasema, “Bwana hataona yatakayotupata sisi.” 5“Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda, unawezaje kushindana na farasi? Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama, utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani? 6Ndugu zako, watu wa jamaa yako mwenyewe: hata wao wamekusaliti; wameinua kilio kikubwa dhidi yako. Usiwaamini, ingawa wanazungumza mema juu yako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.