Yeremia 12:3
Jeremiah 12:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hata hivyo unanijua mimi, Ee Bwana; unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe. Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa! Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa!
Jeremiah 12:3 in English
Jeremiah 12:3 · Berean Standard Bible
But You know me, O LORD; You see me and test my heart toward You. Drag away the wicked like sheep to the slaughter and set them apart for the day of carnage.
Context
1Wewe daima u mwenye haki, Ee Bwana,
niletapo mashtaka mbele yako.
Hata hivyo nitazungumza nawe kuhusu hukumu yako:
Kwa nini njia ya waovu inafanikiwa?
Kwa nini wasio waaminifu
wote wanaishi kwa raha? 2Umewapanda, nao wameota,
wanakua na kuzaa matunda.
Daima u midomoni mwao,
lakini mbali na mioyo yao. 3Hata hivyo unanijua mimi, Ee Bwana;
unaniona na kuyachunguza mawazo yangu kukuhusu wewe.
Wakokote kama kondoo wanaokwenda kuchinjwa!
Watenge kwa ajili ya siku ya kuchinjwa! 4Je, nchi itakaa katika hali ya kuomboleza mpaka lini,
na majani katika kila shamba kunyauka?
Kwa sababu wale waishio ndani yake ni waovu,
wanyama na ndege wameangamia.
Zaidi ya hayo, watu wanasema,
“Bwana hataona yatakayotupata sisi.” 5“Ikiwa umeshindana mbio na watu kwa mguu na wakakushinda,
unawezaje kushindana na farasi?
Ikiwa unajikwaa kwenye nchi ambayo ni salama,
utawezaje kwenye vichaka kando ya Yordani?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.