Native Bible

Jeremiah 12:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu na kulikanyaga shamba langu; watalifanya shamba langu zuri kuwa jangwa la ukiwa.

Jeremiah 12:10 in English

Jeremiah 12:10 · Berean Standard Bible

Many shepherds have destroyed My vineyard; they have trampled My plot of ground. They have turned My pleasant field into a desolate wasteland.

Context

8Urithi wangu umekuwa kwangu kama simba wa msituni. Huningurumia mimi, kwa hiyo ninamchukia. 9Je, urithi wangu haukuwa kama ndege wa mawindo wa madoadoa ambaye ndege wengine wawindao humzunguka na kumshambulia? Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni; walete ili wale. 10Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu na kulikanyaga shamba langu; watalifanya shamba langu zuri kuwa jangwa la ukiwa. 11Litafanywa kuwa jangwa, lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu; nchi yote itafanywa jangwa kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali. 12Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani mharabu atajaa, kwa maana upanga wa Bwana utawala, kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine; hakuna hata mmoja atakayekuwa salama.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.