Yeremia 12:11
Jeremiah 12:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Litafanywa kuwa jangwa, lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu; nchi yote itafanywa jangwa kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali.
Jeremiah 12:11 in English
Jeremiah 12:11 · Berean Standard Bible
They have made it a desolation; desolate before Me, it mourns. All the land is laid waste, but no man takes it to heart.
Context
9Je, urithi wangu haukuwa
kama ndege wa mawindo wa madoadoa
ambaye ndege wengine wawindao
humzunguka na kumshambulia?
Nenda ukawakusanye pamoja wanyama wote wa mwituni;
walete ili wale. 10Wachungaji wengi wataliharibu shamba langu la mizabibu
na kulikanyaga shamba langu;
watalifanya shamba langu zuri
kuwa jangwa la ukiwa. 11Litafanywa kuwa jangwa,
lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu;
nchi yote itafanywa jangwa
kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali. 12Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani
mharabu atajaa,
kwa maana upanga wa Bwana utawala,
kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine;
hakuna hata mmoja atakayekuwa salama. 13Watapanda ngano lakini watavuna miiba;
watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote.
Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako
kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.