Yeremia 12:13
Jeremiah 12:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watapanda ngano lakini watavuna miiba; watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote. Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.”
Jeremiah 12:13 in English
Jeremiah 12:13 · Berean Standard Bible
They have sown wheat but harvested thorns. They have exhausted themselves to no avail. Bear the shame of your harvest because of the fierce anger of the LORD.”
Context
11Litafanywa kuwa jangwa,
lililokauka na kuachwa ukiwa mbele zangu;
nchi yote itafanywa jangwa
kwa sababu hakuna hata mmoja anayejali. 12Juu ya miinuko yote ilivyo kama jangwani
mharabu atajaa,
kwa maana upanga wa Bwana utawala,
kuanzia ncha moja ya nchi hadi nyingine;
hakuna hata mmoja atakayekuwa salama. 13Watapanda ngano lakini watavuna miiba;
watajitaabisha lakini hawatafaidi chochote.
Kwa hiyo beba aibu ya mavuno yako
kwa sababu ya hasira kali ya Bwana Mungu.” 14Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa habari ya majirani zangu wote wabaya wanaonyangʼanya urithi ambao ninawapa watu wangu Israeli, nitawangʼoa kutoka nchi zao, nami nitaingʼoa nyumba ya Yuda kutoka katikati yao. 15Lakini baada ya kuwangʼoa, nitawahurumia tena na kumrudisha kila mmoja wao kwenye urithi wake mwenyewe na kwenye nchi yake mwenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.