Native Bible

Isaiah 8:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Funga ushuhuda na kutia muhuri sheria miongoni mwa wanafunzi wangu.

Isaiah 8:16 in English

Isaiah 8:16 · Berean Standard Bible

Bind up the testimony and seal the law among my disciples.

Context

14naye atakuwa mahali patakatifu; lakini kwa nyumba zote mbili za Israeli atakuwa jiwe lile linalosababisha watu kujikwaa na mwamba wa kuwaangusha. Kwa watu wa Yerusalemu, atakuwa mtego na tanzi. 15Wengi wao watajikwaa; wataanguka na kuvunjika, watategwa na kunaswa.” 16Funga ushuhuda na kutia muhuri sheria miongoni mwa wanafunzi wangu. 17Nitamngojea Bwana, ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake. Nitaliweka tumaini langu kwake. 18Niko hapa, pamoja na watoto ambao Bwana amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayeishi juu ya Mlima Sayuni.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.