Isaya 8:18
Isaiah 8:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Niko hapa, pamoja na watoto ambao Bwana amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayeishi juu ya Mlima Sayuni.
Isaiah 8:18 in English
Isaiah 8:18 · Berean Standard Bible
Here am I, and the children the LORD has given me * as signs and symbols in Israel from the LORD of Hosts, who dwells on Mount Zion.
Context
16Funga ushuhuda na kutia muhuri sheria
miongoni mwa wanafunzi wangu. 17Nitamngojea Bwana,
ambaye ameificha nyumba ya Yakobo uso wake.
Nitaliweka tumaini langu kwake. 18Niko hapa, pamoja na watoto ambao Bwana amenipa. Sisi ni ishara na mfano wake katika Israeli, kutoka kwa Bwana Mwenye Nguvu Zote, anayeishi juu ya Mlima Sayuni. 19Wakati watu wanapowaambia ninyi kutafuta ushauri kwa waaguzi na wenye kuongea na mizimu, ambao hunongʼona na kunungʼunika, je, watu wasingeuliza kwa Mungu wao? Kwa nini watake shauri kwa wafu kwa ajili ya walio hai? 20Kwa sheria na kwa ushuhuda! Kama hawatasema sawasawa na neno hili, hawana mwanga wa mapambazuko.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.