Isaya 5:11
Isaiah 5:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema wakikimbilia kunywa vileo, wale wakawiao sana mpaka usiku, mpaka wamewaka kwa mvinyo.
Isaiah 5:11 in English
Isaiah 5:11 · Berean Standard Bible
Woe to those who rise early in the morning in pursuit of strong drink, who linger into the evening, to be inflamed by wine.
Context
9Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema nikisikia:
“Hakika nyumba kubwa zitakuwa ukiwa,
nayo majumba ya fahari yatabaki bila kukaliwa. 10Shamba la mizabibu la eka kumi
litatoa bathi* moja ya divai,
na homeri* ya mbegu zilizopandwa
itatoa efa* moja tu ya nafaka.” 11Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema
wakikimbilia kunywa vileo,
wale wakawiao sana mpaka usiku,
mpaka wamewaka kwa mvinyo. 12Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao,
matari, filimbi na mvinyo,
lakini hawayajali matendo ya Bwana,
wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake. 13Kwa hiyo watu wangu watakwenda uhamishoni
kwa sababu ya kukosa ufahamu,
watu wao wenye vyeo watakufa kwa njaa
na watu wao wengi watakauka kwa kiu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.