Isaya 5:9
Isaiah 5:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema nikisikia: “Hakika nyumba kubwa zitakuwa ukiwa, nayo majumba ya fahari yatabaki bila kukaliwa.
Isaiah 5:9 in English
Isaiah 5:9 · Berean Standard Bible
I heard the LORD of Hosts declare: “Surely many houses will become desolate, great mansions left unoccupied.
Context
7Shamba la mzabibu la Bwana Mwenye Nguvu Zote
ni nyumba ya Israeli,
na watu wa Yuda
ni bustani yake ya kumpendeza.
Alitazamia haki, lakini akaona umwagaji damu,
alitazamia uadilifu, lakini akasikia vilio vya taabu. 8Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumba
na kuunganisha mashamba baada ya mashamba
hadi hakuna nafasi iliyobaki,
nanyi mnaishi peke yenu katika nchi. 9Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema nikisikia:
“Hakika nyumba kubwa zitakuwa ukiwa,
nayo majumba ya fahari yatabaki bila kukaliwa. 10Shamba la mizabibu la eka kumi
litatoa bathi* moja ya divai,
na homeri* ya mbegu zilizopandwa
itatoa efa* moja tu ya nafaka.” 11Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema
wakikimbilia kunywa vileo,
wale wakawiao sana mpaka usiku,
mpaka wamewaka kwa mvinyo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.