Native Bible

Isaiah 5:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Shamba la mizabibu la eka kumi litatoa bathi* moja ya divai, na homeri* ya mbegu zilizopandwa itatoa efa* moja tu ya nafaka.”

Isaiah 5:10 in English

Isaiah 5:10 · Berean Standard Bible

For ten acres of vineyard will yield but a bath of wine,* and a homer of seed only an ephah of grain.*”

Context

8Ole wenu mnaoongeza nyumba baada ya nyumba na kuunganisha mashamba baada ya mashamba hadi hakuna nafasi iliyobaki, nanyi mnaishi peke yenu katika nchi. 9Bwana Mwenye Nguvu Zote amesema nikisikia: “Hakika nyumba kubwa zitakuwa ukiwa, nayo majumba ya fahari yatabaki bila kukaliwa. 10Shamba la mizabibu la eka kumi litatoa bathi* moja ya divai, na homeri* ya mbegu zilizopandwa itatoa efa* moja tu ya nafaka.” 11Ole wao wale waamkao asubuhi na mapema wakikimbilia kunywa vileo, wale wakawiao sana mpaka usiku, mpaka wamewaka kwa mvinyo. 12Wana vinubi na zeze kwenye karamu zao, matari, filimbi na mvinyo, lakini hawayajali matendo ya Bwana, wala hawana heshima kwa ajili ya kazi ya mikono yake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.