Isaya 49:10
Isaiah 49:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hawataona njaa wala kuona kiu, wala hari ya jangwani au jua halitawapiga. Yeye mwenye huruma juu yao atawaonyesha njia, na kuwaongoza kando ya chemchemi za maji.
Isaiah 49:10 in English
Isaiah 49:10 · Berean Standard Bible
They will not hunger or thirst, nor will scorching heat or sun beat down on them.* For He who has compassion on them will guide them and lead them beside springs of water.
Context
8Hili ndilo asemalo Bwana:
“Wakati wangu uliokubalika nitakujibu,
nami katika siku ya wokovu nitakusaidia;
nitakuhifadhi, nami nitakufanya
kuwa agano kwa ajili ya watu,
ili kurudisha nchi
na kugawanyia urithi tena wale waliokuwa ukiwa, 9kuwaambia mateka, ‘Tokeni nje,’
nao wale walio gizani, ‘Kuweni huru!’
“Watajilisha kando ya barabara
na kupata malisho yao juu ya kila kilima kilicho kitupu. 10Hawataona njaa wala kuona kiu,
wala hari ya jangwani au jua halitawapiga.
Yeye mwenye huruma juu yao atawaonyesha njia,
na kuwaongoza kando ya chemchemi za maji. 11Nitaifanya milima yangu yote kuwa barabara,
na njia kuu zangu zitainuliwa. 12Tazama, watakuja kutoka mbali:
wengine kutoka kaskazini, wengine kutoka magharibi,
wengine kutoka nchi ya Sinimu.”*
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.