Isaya 40:19
Isaiah 40:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu, naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu na kuitengenezea mikufu ya fedha.
Isaiah 40:19 in English
Isaiah 40:19 · Berean Standard Bible
To an idol that a craftsman casts and a metalworker overlays with gold and fits with silver chains?
Context
17Mbele yake mataifa yote ni kama si kitu,
yanaonekana yasio na thamani
na zaidi ya bure kabisa. 18Basi, utamlinganisha Mungu na nani?
Utamlinganisha na kitu gani? 19Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu,
naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu
na kuitengenezea mikufu ya fedha. 20Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii
huuchagua mti usiooza.
Humtafuta fundi stadi
wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika. 21Je, hujui?
Je, hujasikia?
Je, hujaambiwa tangu mwanzo?
Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.