Isaya 40:21
Isaiah 40:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, hujui? Je, hujasikia? Je, hujaambiwa tangu mwanzo? Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia?
Isaiah 40:21 in English
Isaiah 40:21 · Berean Standard Bible
Do you not know? Have you not heard? Has it not been declared to you from the beginning? Have you not understood since the foundation of the earth?
Context
19Kwa habari ya sanamu, fundi huisubu,
naye mfua dhahabu huifunika kwa dhahabu
na kuitengenezea mikufu ya fedha. 20Mtu aliye maskini sana asiyeweza kuleta sadaka kama hii
huuchagua mti usiooza.
Humtafuta fundi stadi
wa kusimamisha sanamu ambayo haitatikisika. 21Je, hujui?
Je, hujasikia?
Je, hujaambiwa tangu mwanzo?
Je, hujafahamu tangu kuumbwa kwa dunia? 22Anakaa kwenye kiti cha enzi juu ya duara ya dunia,
nao watu wakaao ndani yake ni kama panzi.
Huzitandaza mbingu kama chandarua,
na kuzitandaza kama hema la kuishi. 23Huwafanya wakuu kuwa si kitu,
na kuwashusha watawala wa dunia hii kuwa kitu bure.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.