Native Bible

Isaiah 38:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu, je, ni lazima nipite katika malango ya mauti,* na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?”

Isaiah 38:10 in English

Isaiah 38:10 · Berean Standard Bible

I said, “In the prime * of my life I must go through the gates of Sheol and be deprived of the remainder of my years.”

Context

8Nitafanya kivuli cha jua kwenye ngazi iliyojengwa na Ahazi kirudi nyuma madaraja kumi.’ ” Hivyo jua likarudi nyuma madaraja kumi ambayo lilikuwa limeshuka. 9Maandiko ya Hezekia mfalme wa Yuda baada ya kuugua kwake na kupona: 10Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu, je, ni lazima nipite katika malango ya mauti,* na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?” 11Nilisema, “Sitamwona tena Bwana, Bwana katika nchi ya walio hai, wala sitamtazama tena mwanadamu, wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu. 12Kama hema la mchunga mifugo, nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu. Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu, naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi. Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.