Native Bible

Isaiah 38:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nilisema, “Sitamwona tena Bwana, Bwana katika nchi ya walio hai, wala sitamtazama tena mwanadamu, wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu.

Isaiah 38:11 in English

Isaiah 38:11 · Berean Standard Bible

I said, “I will never again see the LORD, even the LORD, in the land of the living; I will no longer look on mankind with those who dwell in this world.

Context

9Maandiko ya Hezekia mfalme wa Yuda baada ya kuugua kwake na kupona: 10Nilisema, “Katika ustawi wa maisha yangu, je, ni lazima nipite katika malango ya mauti,* na kupokonywa miaka yangu iliyobaki?” 11Nilisema, “Sitamwona tena Bwana, Bwana katika nchi ya walio hai, wala sitamtazama tena mwanadamu, wala kuwa na wale ambao sasa wanakaa katika ulimwengu huu. 12Kama hema la mchunga mifugo, nyumba yangu imebomolewa na kutwaliwa kutoka kwangu. Kama mfumaji nimevingirisha maisha yangu, naye amenikatilia mbali kutoka kitanda cha mfumi. Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu. 13Nilingoja kwa uvumilivu hadi mapambazuko, lakini alivunja mifupa yangu yote kama simba. Mchana na usiku uliyakomesha maisha yangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.