Native Bible

Isaiah 33:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake na kuiona nchi inayoenea mbali.

Isaiah 33:17 in English

Isaiah 33:17 · Berean Standard Bible

Your eyes will see the King in His beauty and behold a land that stretches afar.

Context

15Yeye aendaye kwa uadilifu na kusema lililo haki, yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma na kuizuia mikono yake isipokee rushwa, yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji, na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu: 16huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu, ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani. Atapewa mkate wake, na maji yake hayatakoma. 17Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake na kuiona nchi inayoenea mbali. 18Katika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita: “Yuko wapi yule afisa mkuu? Yuko wapi yule aliyechukua ushuru? Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?” 19Hutawaona tena wale watu wenye kiburi, wale watu wenye usemi wa mafumbo, wenye lugha ngeni, isiyoeleweka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.