Isaya 33:16
Isaiah 33:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu, ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani. Atapewa mkate wake, na maji yake hayatakoma.
Isaiah 33:16 in English
Isaiah 33:16 · Berean Standard Bible
he will dwell on the heights; the mountain fortress will be his refuge; his food will be provided and his water assured.
Context
14Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu,
kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu:
“Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao?
Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?” 15Yeye aendaye kwa uadilifu
na kusema lililo haki,
yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma
na kuizuia mikono yake isipokee rushwa,
yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji,
na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu: 16huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu,
ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani.
Atapewa mkate wake,
na maji yake hayatakoma. 17Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake
na kuiona nchi inayoenea mbali. 18Katika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita:
“Yuko wapi yule afisa mkuu?
Yuko wapi yule aliyechukua ushuru?
Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.