Isaya 33:18
Isaiah 33:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita: “Yuko wapi yule afisa mkuu? Yuko wapi yule aliyechukua ushuru? Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?”
Isaiah 33:18 in English
Isaiah 33:18 · Berean Standard Bible
Your mind will ponder the former terror: “Where is he who tallies? Where is he who weighs? Where is he who counts the towers?”
Context
16huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu,
ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani.
Atapewa mkate wake,
na maji yake hayatakoma. 17Macho yenu yatamwona mfalme katika uzuri wake
na kuiona nchi inayoenea mbali. 18Katika mawazo yenu mtaifikiria hofu iliyopita:
“Yuko wapi yule afisa mkuu?
Yuko wapi yule aliyechukua ushuru?
Yuko wapi afisa msimamizi wa minara?” 19Hutawaona tena wale watu wenye kiburi,
wale watu wenye usemi wa mafumbo,
wenye lugha ngeni, isiyoeleweka. 20Mtazame Sayuni, mji wa sikukuu zetu;
macho yenu yatauona Yerusalemu,
mahali pa amani pa kuishi, hema ambalo halitaondolewa,
nguzo zake hazitangʼolewa kamwe,
wala hakuna kamba yake yoyote itakayokatika.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.