Isaya 33:14
Isaiah 33:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu, kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu: “Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao? Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?”
Isaiah 33:14 in English
Isaiah 33:14 · Berean Standard Bible
The sinners in Zion are afraid; trembling grips the ungodly: “Who of us can dwell with a consuming fire? Who of us can dwell with everlasting flames?”
Context
12Mataifa yatachomwa kama ichomwavyo chokaa,
kama vichaka vya miiba vilivyokatwa ndivyo watakavyochomwa.” 13Ninyi mlio mbali sana, sikieni lile nililofanya;
ninyi mlio karibu, tambueni uweza wangu! 14Wenye dhambi katika Sayuni wametiwa hofu,
kutetemeka kumewakumba wasiomcha Mungu:
“Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto ulao?
Ni nani miongoni mwetu awezaye kuishi na moto unaowaka milele?” 15Yeye aendaye kwa uadilifu
na kusema lililo haki,
yeye anayekataa faida ipatikanayo kwa dhuluma
na kuizuia mikono yake isipokee rushwa,
yeye azuiaye masikio yake dhidi ya mashauri ya mauaji,
na yeye afumbaye macho yake yasitazame sana uovu: 16huyu ndiye mtu atakayeishi mahali pa juu,
ambaye kimbilio lake litakuwa ngome ya mlimani.
Atapewa mkate wake,
na maji yake hayatakoma.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.