Native Bible

Isaiah 32:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mpumbavu hataitwa tena muungwana, wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu.

Isaiah 32:5 in English

Isaiah 32:5 · Berean Standard Bible

No longer will a fool be called noble, nor a scoundrel be respected.

Context

3Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena, nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza. 4Moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa, nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha. 5Mpumbavu hataitwa tena muungwana, wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu. 6Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu, moyo wake hushughulika na uovu: Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu, na hueneza habari za makosa kuhusu Bwana; yeye huwaacha wenye njaa bila kitu, na wenye kiu huwanyima maji. 7Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu, hufanya mipango miovu ili kumwangamiza maskini kwa uongo, hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.