Isaya 32:7
Isaiah 32:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu, hufanya mipango miovu ili kumwangamiza maskini kwa uongo, hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki.
Isaiah 32:7 in English
Isaiah 32:7 · Berean Standard Bible
The weapons of the scoundrel are destructive; he hatches plots to destroy the poor with lies, even when the plea of the needy is just.
Context
5Mpumbavu hataitwa tena muungwana,
wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu. 6Kwa kuwa mpumbavu hunena upumbavu,
moyo wake hushughulika na uovu:
Hutenda mambo yasiyo ya kumcha Mungu,
na hueneza habari za makosa kuhusu Bwana;
yeye huwaacha wenye njaa bila kitu,
na wenye kiu huwanyima maji. 7Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu,
hufanya mipango miovu
ili kumwangamiza maskini kwa uongo,
hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki. 8Lakini mtu muungwana hufanya mipango ya kiungwana,
na kwa matendo ya kiungwana yeye hufanikiwa. 9Enyi wanawake wenye kuridhika sana,
amkeni na mnisikilize.
Enyi binti mnaojisikia kuwa salama,
sikieni lile ninalotaka kuwaambia!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.