Isaya 32:9
Isaiah 32:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Enyi wanawake wenye kuridhika sana, amkeni na mnisikilize. Enyi binti mnaojisikia kuwa salama, sikieni lile ninalotaka kuwaambia!
Isaiah 32:9 in English
Isaiah 32:9 · Berean Standard Bible
Stand up, you complacent women; listen to me. Give ear to my word, you overconfident daughters.
Context
7Taratibu za mtu mbaya kabisa ni ovu,
hufanya mipango miovu
ili kumwangamiza maskini kwa uongo,
hata wakati ambapo hoja za mhitaji ni za haki. 8Lakini mtu muungwana hufanya mipango ya kiungwana,
na kwa matendo ya kiungwana yeye hufanikiwa. 9Enyi wanawake wenye kuridhika sana,
amkeni na mnisikilize.
Enyi binti mnaojisikia kuwa salama,
sikieni lile ninalotaka kuwaambia! 10Muda zaidi kidogo ya mwaka mmoja,
ninyi mnaojisikia salama mtatetemeka,
mavuno ya zabibu yatakoma
na mavuno ya matunda hayatakuwepo. 11Tetemekeni, enyi wanawake wenye kuridhika,
tetemekeni kwa hofu, enyi binti mnaojisikia salama!
Vueni nguo zenu,
vaeni nguo ya gunia viunoni mwenu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.