Isaya 32:3
Isaiah 32:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena, nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza.
Isaiah 32:3 in English
Isaiah 32:3 · Berean Standard Bible
Then the eyes of those who see will no longer be closed, and the ears of those who hear will listen.
Context
1Tazama, mfalme atatawala kwa uadilifu
na watawala watatawala kwa haki. 2Kila mtu atakuwa kama kivuli cha kujificha kutokana na upepo
na kimbilio kutokana na dhoruba,
kama vijito vya maji jangwani
na kivuli cha mwamba mkubwa katika ardhi yenye kiu. 3Ndipo macho ya wale wanaoona hayatafumbwa tena,
nayo masikio ya wale wanaosikia yatasikiliza. 4Moyo wa mtu mwenye hamaki utafahamu na kuelewa,
nao ulimi wenye kigugumizi utanena kwa ufasaha. 5Mpumbavu hataitwa tena muungwana,
wala mtu mbaya kabisa kupewa heshima ya juu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.