Isaya 32:16
Isaiah 32:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Haki itakaa katika jangwa, na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba.
Isaiah 32:16 in English
Isaiah 32:16 · Berean Standard Bible
Then justice will inhabit the wilderness, and righteousness will dwell in the fertile field.
Context
14Ngome itaachwa,
mji wenye kelele nyingi utahamwa,
ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele,
mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo, 15mpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu,
nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba,
na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu. 16Haki itakaa katika jangwa,
na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba. 17Matunda ya haki yatakuwa amani,
matokeo ya haki yatakuwa utulivu
na matumaini milele. 18Watu wangu wataishi katika makao ya mahali pa amani,
katika nyumba zilizo salama,
katika mahali pa kupumzika pasipo na usumbufu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.