Native Bible

Isaiah 32:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

mpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu, nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu.

Isaiah 32:15 in English

Isaiah 32:15 · Berean Standard Bible

until the Spirit is poured out upon us from on high. Then the desert will be an orchard, and the orchard will seem like a forest.

Context

13na kwa ajili ya nchi ya watu wangu, nchi ambayo miiba na michongoma imemea: naam, ombolezeni kwa ajili ya nyumba zote za furaha na kwa ajili ya mji huu wenye kufanya sherehe. 14Ngome itaachwa, mji wenye kelele nyingi utahamwa, ngome ndani ya mji na mnara wa ulinzi vitakuwa ukiwa milele, mahali pazuri pa punda na malisho ya makundi ya kondoo, 15mpaka Roho amwagwe juu yetu kutoka juu, nalo jangwa kuwa shamba lenye rutuba, na shamba lenye rutuba kuwa kama msitu. 16Haki itakaa katika jangwa, na uadilifu utakaa katika shamba lenye rutuba. 17Matunda ya haki yatakuwa amani, matokeo ya haki yatakuwa utulivu na matumaini milele.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.