Native Bible

Isaiah 28:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu, kitakanyagwa chini ya nyayo.

Isaiah 28:3 in English

Isaiah 28:3 · Berean Standard Bible

The majestic crown of Ephraim’s drunkards will be trampled underfoot.

Context

1Ole kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu, kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba: kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo! 2Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu. Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo, kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo, atakiangusha chini kwa nguvu. 3Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu, kitakanyagwa chini ya nyayo. 4Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake, uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba, litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno: mara mtu aionapo, huichuma na kuila. 5Katika siku ile, Bwana Mwenye Nguvu Zote atakuwa taji la utukufu, taji zuri la maua kwa mabaki ya watu wake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.