Isaya 28:2
Isaiah 28:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu. Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo, kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo, atakiangusha chini kwa nguvu.
Isaiah 28:2 in English
Isaiah 28:2 · Berean Standard Bible
Behold, the Lord has one who is strong and mighty. Like a hailstorm or destructive tempest, like a driving rain or flooding downpour, he will smash that crown to the ground.
Context
1Ole kwa lile taji la maua, kiburi cha walevi wa Efraimu,
kwa ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,
uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba:
kwa ule mji, kiburi cha wale walioshushwa na mvinyo! 2Tazama, Bwana anaye mmoja aliye na uwezo na nguvu.
Kama dhoruba ya mvua ya mawe na upepo uharibuo,
kama mvua inyeshayo kwa nguvu na mafuriko yashukayo,
atakiangusha chini kwa nguvu. 3Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu,
kitakanyagwa chini ya nyayo. 4Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,
uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,
litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno:
mara mtu aionapo, huichuma na kuila.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.