Isaya 28:5
Isaiah 28:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku ile, Bwana Mwenye Nguvu Zote atakuwa taji la utukufu, taji zuri la maua kwa mabaki ya watu wake.
Isaiah 28:5 in English
Isaiah 28:5 · Berean Standard Bible
On that day the LORD of Hosts will be a crown of glory, a diadem of splendor to the remnant of His people,
Context
3Lile taji la maua, kiburi cha walevi cha Efraimu,
kitakanyagwa chini ya nyayo. 4Lile ua linalosinyaa, uzuri wa utukufu wake,
uliowekwa kwenye kichwa cha bonde lenye rutuba,
litakuwa kama tini iliyoiva kabla ya mavuno:
mara mtu aionapo, huichuma na kuila. 5Katika siku ile, Bwana Mwenye Nguvu Zote
atakuwa taji la utukufu,
taji zuri la maua
kwa mabaki ya watu wake. 6Atakuwa roho ya haki
kwa yeye aketiye katika kiti cha hukumu,
chanzo cha nguvu
kwa wale wazuiao vita langoni. 7Hawa pia wanapepesuka kwa sababu ya mvinyo,
wanayumbayumba kwa sababu ya kileo:
Makuhani na manabii wanapepesuka kwa sababu ya kileo,
wanachanganyikiwa kwa sababu ya mvinyo;
wanapepesuka wanapoona maono,
wanajikwaa wanapotoa maamuzi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.