Isaya 24:7
Isaiah 24:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka, watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni.
Isaiah 24:7 in English
Isaiah 24:7 · Berean Standard Bible
The new wine dries up, the vine withers. All the merrymakers now groan.
Context
5Dunia imetiwa unajisi na watu wake;
wameacha kutii sheria,
wamevunja amri
na kuvunja agano la milele. 6Kwa hiyo laana inaiteketeza dunia,
watu wake lazima waichukue hatia yao.
Kwa hiyo wakazi wa dunia wameteketezwa,
nao waliosalia ni wachache sana. 7Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka,
watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni. 8Furaha ya matoazi imekoma,
kelele za wenye furaha zimekoma,
shangwe za kinubi zimenyamaza. 9Hawanywi tena mvinyo pamoja na wimbo,
kileo ni kichungu kwa wanywaji wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.