Isaya 24:5
Isaiah 24:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Dunia imetiwa unajisi na watu wake; wameacha kutii sheria, wamevunja amri na kuvunja agano la milele.
Isaiah 24:5 in English
Isaiah 24:5 · Berean Standard Bible
The earth is defiled by its people; they have transgressed the laws; they have overstepped the decrees and broken the everlasting covenant.
Context
3Dunia itaharibiwa kabisa
na kutekwa nyara kabisa.
Bwana amesema neno hili. 4Dunia inakauka na kunyauka,
dunia inanyongʼonyea na kunyauka,
waliotukuzwa wa dunia wananyongʼonyea. 5Dunia imetiwa unajisi na watu wake;
wameacha kutii sheria,
wamevunja amri
na kuvunja agano la milele. 6Kwa hiyo laana inaiteketeza dunia,
watu wake lazima waichukue hatia yao.
Kwa hiyo wakazi wa dunia wameteketezwa,
nao waliosalia ni wachache sana. 7Divai mpya inakauka na mzabibu unanyauka,
watu wote wafurahishao wanalia kwa huzuni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.