Isaya 24:3
Isaiah 24:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Dunia itaharibiwa kabisa na kutekwa nyara kabisa. Bwana amesema neno hili.
Isaiah 24:3 in English
Isaiah 24:3 · Berean Standard Bible
The earth will be utterly laid waste and thoroughly plundered. For the LORD has spoken this word.
Context
1Tazama, Bwana ataifanya dunia kuwa ukiwa
na kuiharibu,
naye atauharibu uso wake
na kutawanya wakaao ndani yake: 2ndivyo itakavyokuwa
kwa makuhani na kwa watu,
kwa bwana na kwa mtumishi,
kwa bibi na kwa mtumishi wake wa kike,
kwa muuzaji na kwa mnunuzi,
kwa mkopaji na kwa mkopeshaji,
kwa mdaiwa na kwa mdai. 3Dunia itaharibiwa kabisa
na kutekwa nyara kabisa.
Bwana amesema neno hili. 4Dunia inakauka na kunyauka,
dunia inanyongʼonyea na kunyauka,
waliotukuzwa wa dunia wananyongʼonyea. 5Dunia imetiwa unajisi na watu wake;
wameacha kutii sheria,
wamevunja amri
na kuvunja agano la milele.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.