Native Bible

Isaiah 14:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli: Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho! Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma!

Isaiah 14:4 in English

Isaiah 14:4 · Berean Standard Bible

you will sing this song of contempt against the king of Babylon: How the oppressor has ceased, and how his fury * has ended!

Context

2Mataifa watawachukua na kuwaleta mahali pao wenyewe. Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana. Watawafanya watekaji wao kuwa mateka, na kutawala juu ya wale waliowaonea. 3Katika siku Bwana atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili, 4utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli: Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho! Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma! 5Bwana amevunja fimbo ya mwovu, fimbo ya utawala ya watawala, 6ambayo kwa hasira waliyapiga mataifa kwa mapigo yasiyo na kikomo, nao kwa ghadhabu kali waliwatiisha mataifa kwa jeuri pasipo huruma.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.