Isaya 14:3
Isaiah 14:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika siku Bwana atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili,
Isaiah 14:3 in English
Isaiah 14:3 · Berean Standard Bible
On the day that the LORD gives you rest from your pain and torment, and from the hard labor into which you were forced,
Context
1Bwana atamhurumia Yakobo,
atamchagua Israeli tena,
na kuwakalisha katika nchi yao wenyewe.
Wageni wataungana nao
na kujiunga na nyumba ya Yakobo. 2Mataifa watawachukua
na kuwaleta mahali pao wenyewe.
Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa
kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana.
Watawafanya watekaji wao kuwa mateka,
na kutawala juu ya wale waliowaonea. 3Katika siku Bwana atakapokuondolea mateso, udhia na utumwa wa kikatili, 4utaichukua dhihaka hii dhidi ya mfalme wa Babeli:
Tazama jinsi mtesi alivyofikia mwisho!
Tazama jinsi ghadhabu yake kali ilivyokoma! 5Bwana amevunja fimbo ya mwovu,
fimbo ya utawala ya watawala,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.