Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mimi ni kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa watu wa Yuda.

Hosea 5:12 in English

Hosea 5:12 · Berean Standard Bible

So I am like a moth to Ephraim, and like decay to the house of Judah.

Context

10Viongozi wa Yuda ni kama wale wanaosogeza mawe ya mpaka. Nitamwaga ghadhabu yangu juu yao kama mafuriko ya maji. 11Efraimu ameonewa, amekanyagwa katika hukumu kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu. 12Mimi ni kama nondo kwa Efraimu, na kama uozo kwa watu wa Yuda. 13“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake, naye Yuda vidonda vyake, ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru, na kuomba msaada kwa mfalme mkuu. Lakini hawezi kukuponya, wala hawezi kukuponya vidonda vyako. 14Kwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu, kama simba mkubwa kwa Yuda. Nitawararua vipande vipande na kuondoka; nitawachukua mbali, na hakuna wa kuwaokoa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.