Hosea 5:11
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Efraimu ameonewa, amekanyagwa katika hukumu kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu.
Hosea 5:11 in English
Hosea 5:11 · Berean Standard Bible
Ephraim is oppressed, crushed in judgment, for he is determined to follow worthless idols.*
Context
9Efraimu ataachwa ukiwa
katika siku ya kuadhibiwa.
Miongoni mwa makabila ya Israeli
ninatangaza lile ambalo halina budi kutukia. 10Viongozi wa Yuda ni kama wale
wanaosogeza mawe ya mpaka.
Nitamwaga ghadhabu yangu juu yao
kama mafuriko ya maji. 11Efraimu ameonewa,
amekanyagwa katika hukumu
kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu. 12Mimi ni kama nondo kwa Efraimu,
na kama uozo kwa watu wa Yuda. 13“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake,
naye Yuda vidonda vyake,
ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru,
na kuomba msaada kwa mfalme mkuu.
Lakini hawezi kukuponya,
wala hawezi kukuponya vidonda vyako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.