Hosea 5:13
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake, naye Yuda vidonda vyake, ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru, na kuomba msaada kwa mfalme mkuu. Lakini hawezi kukuponya, wala hawezi kukuponya vidonda vyako.
Hosea 5:13 in English
Hosea 5:13 · Berean Standard Bible
When Ephraim saw his sickness and Judah his wound, then Ephraim turned to Assyria and sent to the great king.* But he cannot cure you or heal your wound.
Context
11Efraimu ameonewa,
amekanyagwa katika hukumu
kwa kuwa amekusudia kufuatia sanamu. 12Mimi ni kama nondo kwa Efraimu,
na kama uozo kwa watu wa Yuda. 13“Wakati Efraimu alipoona ugonjwa wake,
naye Yuda vidonda vyake,
ndipo Efraimu alipogeukia Ashuru,
na kuomba msaada kwa mfalme mkuu.
Lakini hawezi kukuponya,
wala hawezi kukuponya vidonda vyako. 14Kwa maana nitakuwa kama simba kwa Efraimu,
kama simba mkubwa kwa Yuda.
Nitawararua vipande vipande na kuondoka;
nitawachukua mbali,
na hakuna wa kuwaokoa. 15Kisha nitarudi mahali pangu
mpaka watakapokubali kosa lao.
Nao watautafuta uso wangu;
katika taabu yao watanitafuta kwa bidii.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.