Native Bible

Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu* pataharibiwa: ndiyo dhambi ya Israeli. Miiba na mibaruti itaota na kufunika madhabahu zao. Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!” na vilima, “Tuangukieni!”

Hosea 10:8 in English

Hosea 10:8 · Berean Standard Bible

The high places of Aven * will be destroyed— it is the sin of Israel; thorns and thistles will overgrow their altars. Then they will say to the mountains, “Cover us!” and to the hills, “Fall on us!”*

Context

6Itachukuliwa kwenda Ashuru kama ushuru kwa mfalme mkuu. Efraimu atafedheheshwa; Israeli ataaibika kwa ajili ya sanamu zake za mti. 7Samaria na mfalme wake wataelea kama kijiti juu ya uso wa maji. 8Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu* pataharibiwa: ndiyo dhambi ya Israeli. Miiba na mibaruti itaota na kufunika madhabahu zao. Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!” na vilima, “Tuangukieni!” 9“Tangu siku za Gibea, mmetenda dhambi, ee Israeli, huko ndiko mlikobaki. Je, vita havikuwapata watenda mabaya huko Gibea? 10Wakati nitakapopenda, nitawaadhibu; mataifa yatakusanywa dhidi yao ili kuwaweka katika vifungo kwa ajili ya dhambi zao mbili.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.