Hosea 10:9
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Tangu siku za Gibea, mmetenda dhambi, ee Israeli, huko ndiko mlikobaki. Je, vita havikuwapata watenda mabaya huko Gibea?
Hosea 10:9 in English
Hosea 10:9 · Berean Standard Bible
Since the days of Gibeah you have sinned, O Israel, and there you have remained. Did not the battle in Gibeah overtake the sons of iniquity?*
Context
7Samaria na mfalme wake wataelea
kama kijiti juu ya uso wa maji. 8Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu* pataharibiwa:
ndiyo dhambi ya Israeli.
Miiba na mibaruti itaota
na kufunika madhabahu zao.
Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!”
na vilima, “Tuangukieni!” 9“Tangu siku za Gibea, mmetenda dhambi, ee Israeli,
huko ndiko mlikobaki.
Je, vita havikuwapata
watenda mabaya huko Gibea? 10Wakati nitakapopenda, nitawaadhibu;
mataifa yatakusanywa dhidi yao
ili kuwaweka katika vifungo
kwa ajili ya dhambi zao mbili. 11Efraimu ni mtamba wa ngʼombe aliyefundishwa
ambaye hupenda kupura,
hivyo nitamfunga nira
juu ya shingo yake nzuri.
Nitamwendesha Efraimu,
Yuda lazima alime,
naye Yakobo lazima avunjavunje
mabonge ya udongo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.