Hosea 10:6
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Itachukuliwa kwenda Ashuru kama ushuru kwa mfalme mkuu. Efraimu atafedheheshwa; Israeli ataaibika kwa ajili ya sanamu zake za mti.
Hosea 10:6 in English
Hosea 10:6 · Berean Standard Bible
Yes, it will be carried to Assyria as tribute to the great king.* Ephraim * will be seized with shame; Israel will be ashamed of its wooden idols.*
Context
4Wanaweka ahadi nyingi,
huapa viapo vya uongo
wanapofanya mapatano;
kwa hiyo mashtaka huchipuka
kama magugu ya sumu
katika shamba lililolimwa. 5Watu wanaoishi Samaria huogopa
kwa ajili ya sanamu ya ndama ya Beth-Aveni.*
Watu wake wataiombolezea,
vivyo hivyo kuhani wake wa kuabudu sanamu,
wale waliokuwa wamefurahia fahari yake,
kwa sababu itaondolewa kutoka kwao
kwenda uhamishoni. 6Itachukuliwa kwenda Ashuru
kama ushuru kwa mfalme mkuu.
Efraimu atafedheheshwa;
Israeli ataaibika kwa ajili ya sanamu zake za mti. 7Samaria na mfalme wake wataelea
kama kijiti juu ya uso wa maji. 8Mahali pa kuabudia sanamu pa uovu* pataharibiwa:
ndiyo dhambi ya Israeli.
Miiba na mibaruti itaota
na kufunika madhabahu zao.
Kisha wataiambia milima, “Tufunikeni!”
na vilima, “Tuangukieni!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.