Hosea 10:5
Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu wanaoishi Samaria huogopa kwa ajili ya sanamu ya ndama ya Beth-Aveni.* Watu wake wataiombolezea, vivyo hivyo kuhani wake wa kuabudu sanamu, wale waliokuwa wamefurahia fahari yake, kwa sababu itaondolewa kutoka kwao kwenda uhamishoni.
Hosea 10:5 in English
Hosea 10:5 · Berean Standard Bible
The people of Samaria will fear for the calf of Beth-aven.* Indeed, its people will mourn with its idolatrous priests— those who rejoiced in its glory— for it has been taken from them into exile.
Context
3Kisha watasema, “Hatuna mfalme
kwa sababu hatukumheshimu Bwana.
Lakini hata kama tungelikuwa na mfalme,
angeweza kutufanyia nini?” 4Wanaweka ahadi nyingi,
huapa viapo vya uongo
wanapofanya mapatano;
kwa hiyo mashtaka huchipuka
kama magugu ya sumu
katika shamba lililolimwa. 5Watu wanaoishi Samaria huogopa
kwa ajili ya sanamu ya ndama ya Beth-Aveni.*
Watu wake wataiombolezea,
vivyo hivyo kuhani wake wa kuabudu sanamu,
wale waliokuwa wamefurahia fahari yake,
kwa sababu itaondolewa kutoka kwao
kwenda uhamishoni. 6Itachukuliwa kwenda Ashuru
kama ushuru kwa mfalme mkuu.
Efraimu atafedheheshwa;
Israeli ataaibika kwa ajili ya sanamu zake za mti. 7Samaria na mfalme wake wataelea
kama kijiti juu ya uso wa maji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.