Waebrania 5:9
Hebrews 5:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
na akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii.
Hebrews 5:9 in English
Hebrews 5:9 · Berean Standard Bible
And having been made perfect, He became the source of eternal salvation to all who obey Him
Context
7Katika siku za maisha ya Yesu hapa duniani, alimtolea maombi na dua pamoja na kulia sana na machozi, yeye awezaye kumwokoa na mauti, naye Mungu akamsikia kwa sababu ya kutii kwake kwa unyenyekevu. 8Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utiifu kutokana na mateso aliyoyapata, 9na akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii. 10Naye amewekwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki. 11Tunayo mengi ya kusema kuhusu habari ya ukuhani huu, lakini ni vigumu kuyaeleza, kwa sababu ninyi ni wazito wa kuelewa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.