Native Bible

Hebrews 5:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Naye amewekwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki.

Hebrews 5:10 in English

Hebrews 5:10 · Berean Standard Bible

and was designated by God as high priest in the order of Melchizedek.

Context

8Ingawa alikuwa Mwana, alijifunza utiifu kutokana na mateso aliyoyapata, 9na akiisha kukamilishwa, akawa chanzo cha wokovu wa milele kwa wote wanaomtii. 10Naye amewekwa na Mungu kuwa Kuhani Mkuu kwa mfano wa Melkizedeki. 11Tunayo mengi ya kusema kuhusu habari ya ukuhani huu, lakini ni vigumu kuyaeleza, kwa sababu ninyi ni wazito wa kuelewa. 12Kwa hakika, ingawa mpaka wakati huu ingewapasa kuwa walimu, bado mnahitaji mtu wa kuwafundisha tena hatua za awali za kweli ya Neno la Mungu. Mnahitaji maziwa, wala si chakula kigumu!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.