Native Bible

Habakkuk 3:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni katika mngʼao wa mishale yako inayoruka, na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao.

Habakkuk 3:11 in English

Habakkuk 3:11 · Berean Standard Bible

Sun and moon stood still in their places at the flash of Your flying arrows, at the brightness of Your shining spear.

Context

9Uliufunua upinde wako na kuita mishale mingi. Uliigawa dunia kwa mito; 10milima ilikuona ikatetemeka. Mafuriko ya maji yakapita huko; vilindi vilinguruma na kuinua mawimbi yake juu. 11Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni katika mngʼao wa mishale yako inayoruka, na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao. 12Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia, na katika hasira ulikanyaga mataifa. 13Ulikuja kuwaokoa watu wako, kumwokoa uliyemtia mafuta. Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu, ukamvua toka kichwani hadi wayo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.