Habakuki 3:12
Habakkuk 3:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia, na katika hasira ulikanyaga mataifa.
Habakkuk 3:12 in English
Habakkuk 3:12 · Berean Standard Bible
You marched across the earth with fury; You threshed the nations in wrath.
Context
10milima ilikuona ikatetemeka.
Mafuriko ya maji yakapita huko;
vilindi vilinguruma
na kuinua mawimbi yake juu. 11Jua na mwezi vilisimama kimya mbinguni
katika mngʼao wa mishale yako inayoruka,
na katika mngʼao wa mkuki wako umeremetao. 12Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia,
na katika hasira ulikanyaga mataifa. 13Ulikuja kuwaokoa watu wako,
kumwokoa uliyemtia mafuta.
Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu,
ukamvua toka kichwani hadi wayo. 14Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake
wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya,
wakifurahi kama walio karibu kutafuna
wale wanyonge waliokuwa mafichoni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.