Native Bible

Habakkuk 3:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya, wakifurahi kama walio karibu kutafuna wale wanyonge waliokuwa mafichoni.

Habakkuk 3:14 in English

Habakkuk 3:14 · Berean Standard Bible

With his own spear You pierced his head, when his warriors stormed out to scatter us, gloating as though ready to secretly devour the weak.

Context

12Kwa ghadhabu ulipita juu ya dunia, na katika hasira ulikanyaga mataifa. 13Ulikuja kuwaokoa watu wako, kumwokoa uliyemtia mafuta. Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu, ukamvua toka kichwani hadi wayo. 14Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya, wakifurahi kama walio karibu kutafuna wale wanyonge waliokuwa mafichoni. 15Ulikanyaga bahari kwa farasi wako, ukisukasuka maji makuu. 16Nilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu, midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti; uchakavu ukanyemelea mifupa yangu, na miguu yangu ikatetemeka. Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa kuyajilia mataifa yaliyotuvamia.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.