Habakuki 3:15
Habakkuk 3:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ulikanyaga bahari kwa farasi wako, ukisukasuka maji makuu.
Habakkuk 3:15 in English
Habakkuk 3:15 · Berean Standard Bible
You trampled the sea with Your horses, churning the great waters.
Context
13Ulikuja kuwaokoa watu wako,
kumwokoa uliyemtia mafuta.
Ulimponda kiongozi wa nchi ya uovu,
ukamvua toka kichwani hadi wayo. 14Kwa mkuki wake mwenyewe ulitoboa kichwa chake
wakati mashujaa wake walifurika nje kwa kishindo kututawanya,
wakifurahi kama walio karibu kutafuna
wale wanyonge waliokuwa mafichoni. 15Ulikanyaga bahari kwa farasi wako,
ukisukasuka maji makuu. 16Nilisikia na moyo wangu ukagonga kwa nguvu,
midomo yangu ikatetemeka kwa hofu niliposikia sauti;
uchakavu ukanyemelea mifupa yangu,
na miguu yangu ikatetemeka.
Hata hivyo nitasubiri kwa uvumilivu siku ya maafa
kuyajilia mataifa yaliyotuvamia. 17Ingawa mtini hauchanui maua
na hakuna zabibu juu ya mizabibu,
ingawaje mzeituni hauzai,
na hata mashamba hayatoi chakula,
iwapo hakuna kondoo katika banda,
wala ngʼombe katika zizi,
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.