Mwanzo 49:26
Genesis 49:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Baraka za baba yako ni kubwa kuliko baraka za milima ya kale, nyingi kuliko vilima vya kale. Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu, juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake.
Genesis 49:26 in English
Genesis 49:26 · Berean Standard Bible
The blessings of your father have surpassed the blessings of the ancient mountains * and the bounty of the everlasting hills. May they rest on the head of Joseph, on the brow of the prince of his brothers.
Context
24Lakini upinde wake ulibaki imara,
mikono yake ikatiwa nguvu,
na mkono wa Mwenye Nguvu wa Yakobo,
kwa sababu ya Mchungaji, Mwamba wa Israeli, 25kwa sababu ya Mungu wa baba yako, anayekusaidia,
kwa sababu ya Mwenyezi,* yeye anayekubariki
kwa baraka za mbinguni juu,
baraka za kilindi kilichoko chini,
baraka za matitini na za tumbo la uzazi. 26Baraka za baba yako ni kubwa
kuliko baraka za milima ya kale,
nyingi kuliko vilima vya kale.
Baraka hizo zote na zikae juu ya kichwa cha Yosefu,
juu ya paji la yule mkuu miongoni mwa ndugu zake. 27“Benyamini ni mbwa mwitu mlafi mwenye njaa kuu;
asubuhi hurarua mawindo yake,
jioni hugawa nyara.” 28Haya yote ndiyo makabila kumi na mawili ya Israeli, na hivi ndivyo baba yao alivyowaambia alipowabariki, akimpa kila mmoja baraka inayomfaa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.